Ndugu Wanachama wa CRDB Workers SACCOS,
Napenda kuwaarifu kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka 2021 umepangwa kufanyika tarehe 23/10/2021 Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi uliopo NHC House ghorofa ya pili (tulipofanyia Mkutano Mkuu wa mwaka 2020). Mkutano huu unafanyika kwa mujibu wa kanuni ya 42 ya Sheria ya Ushirika na Masharti ya CRDB Workers SACCOS.
Mkutano utaanza saa saba na nusu mchana (13:30 hrs)
Ajenda za Mkutano
1. Kuthibitisha Tangazo la Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021
2. Kuthibitisha Akidi.
3. Kufungua Mkutano.
4. Kuchagua Mwenyekiti wa Mkutano.
5. Kupokea na kuidhinisha wanachama wapya.
6. Kupokea na Kujadili Muhutasari wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2020.
7. Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa Mwaka 2020.
8. Kupokea na Kujadili Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi.
9. Kupokea na Kujadili Taarifa ya Kamati ya Usimamizi.
10. Kupokea na kujadili taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka 2020.
11. Kupokea na kujadili Makisio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2022.
12. Kupokea na kujadili taarifa ya Ombi la Ukomo wa Madeni.
13. Mengineyo.
Tafadhali upatapo tangazo hili wajulishe wanachama wengine.
Aidha tangazo hili linapatikana kwenye tovuti yetu ya chama: www.crdbsaccos.co.tz
“SACCOS pamoja tujenge uchumi”
Lusekelo .A. Kalemela,
Mwenyekiti wa Bodi,
CRDB WORKERS SACCOS LTD.